TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUTOKA MKOA WA MWANZA
TAREHE
19.02.2017 MAJIRA YA SAA 7:25HRS ASUBUHI KATIKA STANDI YA KAMANGA FERI
KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA
ALIYEJULIKANA KWA JINA LA STANSLAUS LUCAS, MIAKA 38 MKURYA NA MKAZI WA
NYAKATO NATIONAL, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA
KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31, KITENDO
AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA
KUWA MTUHUMIWA ALIFIKA HAPO KWENYE STANDI YA KAMANGA FERI MAJIRA TAJWA
HAPO JUU AKIWA NA GARI LENYE NAMBA T.701 AINA YA NOAH, KISHA ALITOA
BOKSI MOJA KUTOKA NDANI YA GARI LAKE NA KUWAKABIDHI MAWAKALA WA MAGARI
YAENDAYO KIGOMA NA KUWAELEZA KUWA MZIGO WAKE ANAOMBA USHUSHWE KIBONDO.
MAWAKALA WA MAGARI WALIPATA MASHAKA JUU YA HILO BOKSI NDIPO WALIMWOMBA
MTUHUMIWA AWAELEZE KITU ALICHOKIWEKA NDANI YA BOKSI, LAKINI MTUHUMIWA
HAKUWEZA KUELEZA KITU CHOCHOTE, NDIPO WALILIFUNGUA NA KULICHEKI NDANI
NA KUONA LIKIWA LIMEJAA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI.
AIDHA
BAADA BOKSI KUONEKANA LIKIWA LIMEWEKWA MIRUNGI, MAWAKALA WA MAAGARI
WALIMSHIKILIA MTUHUMIWA KISHA WAKATOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO
HILO, ASKARI WALIFIKA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANIKIWA KUMTIA
NGUVUNI MTUHUMIWA PAMOJA NA KULIIFANYIA UPEKUZI GARI LAKE AMBAPO
LILIKAMATWA BOKSI LINGINE LIKIWA NA MIRUNGI, AIDHA MABOKSI YOTE MAWILI
YALIYOKAMATWA YALIKUWA NA MIRUNGI KIASI CHA KILO 31.
KATIKA
MAHOJIANO YA AWALI ALIYOFANYIWA MTUHUMIWA NA POLISI ALIKIRI KUWA NI
KWELI AMEKUWA AKIJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA YA AINA YA
MIRUNGI KWA MUDA MREFU, ALIDAI KUWA MIRUNGI AMEKUWA AKIITOLEA SIRARI NA
KUISAMBAZA SEHEMU MBALIMBALI YA JIJI LA MWANZA NA MAENEO YA JIRANI,
LAKINI ALIDAI KUWA MIRUNGI HIYO ALIYOKAMATWA NAYO ALIKUWA AKITAKA
KUISAFIRISHA KWENDA KIBONDO MKOANI KIGOMA. POLISI WANAENDELEA NA
MAHOJIANO NA MTUHUMIWA ILI KUWEZA KUBAINI MTANDAO WA WATU WENGINE
ANAOSHIRIKIANA NAO KATIKA BIASHARA HIYO HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI
ANAWAPONGEZA MAWAKALA WA MAGARI WOTE WA STANDI YA KAMANGA FERI KWA
USHIRIKIANO MZURI WA KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA MADAWA YA KULEVYA AMBAO
WAMEUONESHA KWA WANANCHI, HIVYO ANAWASIHI WATU WOTE WA JIJI LA MWANZA
WAIGE MFANO WA AINA KAMA HII. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WAKAZI WA
JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI
LA POLISI JUU YA WATU WOTE WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA, UTUMIAJI NA
USAFIRISHAJI WA MADAWA HARAMU YA KULEVYA, ILI WAWEZE KUKAMATWA NA
KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO SHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MANAMO
TAREHE 18.02.2017 MAJIRA YA SAA 21:05HRS USIKU KATIKA MTAA WA IGOMBE
KATA YA BUGOGWA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKI
KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WATATU WALIOJULIKANA
KWA MAJINA YA 1. HAJI IDD MIAKA 34, MNYAMWEZI NA MKAZI WA IGOMBE AKIWA
NA BHANGI MISOKOTO 40, 2. VUMILIA CHARLES MIAKA 36, MSUKUMA NA MKAZI WA
IGOMBE AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KIASI CHA LITA 10 NA 3.LEAH GILIGHA
MIAKA 53, MSUKUMA NA MKAZI WA IGOMBE AKIWA NA POMBE AINA YA GONGO KIASI
CHA LITA 06, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI
POLISI WAKIWA KWENYE DORIA NA MIASKO WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA
WEMA JUU YA UWEPO WA WATU KATIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU AMBAO
WANAJIHUSISHA NA BIASHA HARAMU YA POMBE AINA YA GONGO PAMOJA NA BHANGI.
ASKARI WALIFANYA UPELELEZI KATIKA MAENEO HAYO NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA
WATUHUMIWA WATATU TAJWA HAPO JUU, AMBAPO WAWILI WALIKAMATWA WAKIWA NA
POMBE AINA YA GONGO HUKU MMOJA AKIWA NA MISOKOTO YA BHANGI.
POLISI
BADO WANAENDELEA NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI
UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WATATU WATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA
STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAO. AIDHA ASKARI BADO WANAENDELEA NA
UPELELEZI NA MISAKO KATIKA MAENEO HAYO ILI KUWEZA KUWAKAMATA WATU
WENGINE AMBAO WANADAIWA KUWA WANAENDELEA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU
YA POMBE AINA GONGO NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI NA MIRUNGI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA
WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA
KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA MADAWA YA KULEVYA PAMOJA NA POMBE AINA
YA GONGO KWANI NI KOSA LA JINAI, BALI ANAWATAKA WANANCHI WAFANYE KAZI
ZILIZO HALALI ILI WAWEZE KUJIEPUSHA NA MATATIZO, AIDHA ANAENDELEA
KUWATAKA WANANCHI WOTE WA JIJI LA MWANZA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA
JESHI LAO ILI LIWEZE KUDHIBITI VYEMA UHALIFU KATIKA MKOA WETU WA
MWANZA.
IMETOLEWA NA;
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
No comments: